Back to top

Vijana wa JKT waliorejeshwa majumbani watakiwa kuripoti makambini.

30 April 2021
Share

Mkuu wa Jeshi La Kujenga Taifa (JKT) ameutaarifu umma wa watanzania kuwa vijana waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa kujitolea kwa mwaka 2020/2021 ambao mapema mwezi februari mwaka huu walirejeshwa majumbani waanze kuripoti makambini walipokuwa wamepangiwa awali kuanzia Tarehe 7 hadi 14 Mei, 2021. 
.
Akitoa taarifa hiyo kwa umma katika ofisi za makao makuu ya Jeshi La Kujenga Taifa mkoani Dodoma Kaimu Mkuu wa Utawala Kanali Hassan Mabena amewataja vijana wanaotakiwa kuripoti kuwa ni wale wenye elimu ya Darasa la Saba na elimu ya Kidato cha nne.

Aidha, Kaimu Mkuu wa Utawala Kanali Hassan Mabena amesema vijana wenye elimu ya kidato cha sita, ngazi ya cheti, stashahada na wale wenye taaluma ya uhandisi wataendelea kusubiri majumbani hadi hapo utaratibu mwingine utakapotangazwa.