Back to top

Vijana waaswa kutoibua na kuchochea migogoro isiyo ya lazima

26 June 2020
Share

Vijana nchini wameaswa kutojihusisha na migogoro isiyo kuwa ya lazima inayochangia upotevu wa muda,fedha na rasilimali za taifa katika kuitafutia ufumbuzi na badala yake wafanye shughuli za uzalishaji mali

Hayo yamebainishwa wakati wa hitimisho la mafunzo kwa vijana zaidi ya 60 wa mkoa wa Mwanza yaliyolenga kuhamasisha uangalizi wa jamii pamoja na kutatua migogoro kwenye jamii yaliyotolewa na shirika la mfumo na muundo wa muungano wa jamii Tanzania (MUJATA).

Nao baadhi ya washiriki waliopatiwa mafunzo hayo wamesema miongoni mwa watu wanaopitia changamoto ya migogoro ni wanawake ambao wamekuwa wakinyanyasika.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Muliro Jumanne Muliro amesema elimu hiyo itasaidia kuwabadilisha vijana kuacha vitendo vya uhalifu.