Serikali imeombwa kuwachukulia hatua za kinidhamu vijana wanaokwepa kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa sheria kwani kufanya hivyo ni kukaidi utaratibu uliowekwa na serikali.
.
Hayo yamesemwa katika ufungaji wa mafunzo ya vijana wa mujibu wa sheria katika kikosi cha 841 mafinga ambako vijana hao wamesema mafunzo ya yamewasaidia.
.
Kanali Issa Chalamila ni mkuu wa kikosi cha jeshi hilo la 841 Mafinga na Saad Mtambule mkuu wa wilaya ya Mufindi wamesema lazima mafunzo hayo yapewe kipaumbele.
.
Jumla ya vijana 1443 wa mujibu wa sheria operesheni Samia Suluhu 2021 wamehitimu mafunzo ya awali ya kijeshi katika kambi ya jeshi (JKT) Mafinga