Back to top

Vijana Zimbabwe wanavyohatarisha maisha yao.

27 April 2022
Share

Msemaji wa Wizara ya afya nchini Zimbabwe Donald Mujiri amesema wizara hiyo inaifanyia kazi taarifa ya uwepo wa baadhi ya vijana nchini humo wanaodaiwa kutumia kemikali 'sodium polyacrylate' zinazopatikana kwenye nepi (diapers) na taulo za kike mpya au zilizotumika na kuzitumia kama kilevi cha bei nafuu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la For Youths by Youths, amesema  kuwa linafanya kazi na Polisi wa Jamhuri ya Zimbabwe kufuatilia matumizi mabaya ya dawa za kulevya katika jamii na kuwezesha kukamatwa kwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya.

Jena amesema kuna changamoto ya kisheria ambayo vijana wanajinufaisha nayo "Pengo linakuwa kubwa katika polyacrylate ya sodium kwa sababu nepi (diapers) au pedi ni bidhaa halali zinazopatikana kila mahali katika jamii hivyo kuna kaugumu katika kupambana na hili.