Back to top

VIJIJI VYOTE KUFIKIWA NA UMEME IFIKAPO DISEMBA

22 May 2023
Share

Serikali imesema kufikia mwezi Disemba mwaka huu Vijiji vyote nchini, vitakuwa vimefikiwa na umeme, wakati serikali inapoendelea na juhudi za kutafuta fedha ili kufikia kila kitongoji na maeneo yote muhimu yanayohitaji umeme.

Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Stephen Byabato, ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma, akijibu maswali ya wabunge kuhusu changamoto za upatikanaji wa umeme katika maeneo yao.

Kuhusu changamoto ya upatikanaji wa umeme hafifu katika baadhi ya maeneo, Mhe.Byabato amesema tatizo hilo ni la kawaida katika matumizi ya umeme, na hutokea wakati watumiaji wa umeme wanapoongezeka katika eneo husika na mifumo kuzidiwa.

Picha kwa hisani ya Maktaba

Amesema katika kutatua tatizo hilo serikali imetenga fedha kwa ajili ya kulitatua kwa kuongeza vifaa mahsusi zikiwemo Transfoma kubwa, ili kusukuma umeme mwingi na kuwafikia wahitaji.