Back to top

Vilio majonzi vyatawala mazishi ya wanafunzi watano Ruvuma.

14 February 2020
Share

Vilio na majozi vimetawala kwenye mazishi ya wanafunzi watano wa shule ya msingi Ndelenyuma waliofariki dunia kwa kugongwa na gari ambao wamezikwa kwenye  kijijiji cha Ndelenyuma wilayani Songea mkoani Ruvuma.
 
Akiwaongoza waombolezaji kwenye mazishi hayo ya wanafunzi waliopoteza maisha kwa kugongwa na gari aina ya Toyota landcruiser mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bi. Christina Mndeme amewataka madereva kuheshimu sheria za barabarani.