Back to top

Viongozi wa Afrika watakiwa kutambua umuhimu wa nchi zao kuwa na amani

18 May 2018
Share

Marais watatu wastaafu wa Afrika Mhe.Thabo Mbeki, Mhe.Benjamin Mkapa na Mhe.Hassan Sheikh Mohamud, wamewataka viongozi wa sasa wa nchi za Bara la Afrika kutambua umuhimu wa nchi zao kuwa na amani kwa manufaa ya bara hilo.

Wametoa kauli hiyo wakati wa kuhitimisha kongamano la kikanda la viongozi wastaafu wa Afrika kuhusu nafasi ya Afrika katika amani na usalama ulimwenguni.

Wamesema moja kati ya mambo ya msingi ambayo yatasababisha nchi hizo ziwe na amani ni viongozi wa mataifa hayo kutambua umuhimu wa kuheshimu katiba za nchi zao.

Mbali na hilo viongozi wa mataifa yote Barani Afrika wametakiwa kuridhia nchi zao kujiunga na mpango wa kujitathmini wa nchi za Afrika - APRM ambao umezifanya nchi wanachama kuwa vinara Barani Afrika kwa uongozi bora.

Mapendekezo yote ya kongamano hilo yatawasilishwa kamisheni ya umoja wa Afrika nchini Ethiopia.