Back to top

Viongozi wa dunia waapa kuilinda amani ya Libya maradufu.

20 January 2020
Share

Viongozi wa dunia wameapa kuhakikisha kuwa amani ya kudumu inarejea nchini Libya, baada ya kufungua mkutano wa amani kuhusu nchi hiyo jijini Berlin nchini Ujerumani hapo jana Jumapili Januari 19.

Rais wa Uturuki, Ufaransa, Urusi na mwenyeji wao Kansela Angela Merkel ni miongoni mwa wakuu hao waliohudhuria mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na kiongozi wa wapiganaji wa upinzani KHALIFA HAFTAR na kiongozi wa serikali inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa FAYEZ AL-SARRAJ.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Maataifa Antonio Guteress ameyataka mataifa ya kigeni kuacha kuchochea vita nchini Libya kwa kutuma silaha na wanajeshi.

Sambamba na hilo Viongozi wa nchi kuu zinazohusika katika mzozo nchini Libya wamekubaliana kuheshimu vikwazo vya silaha vilivyowekwa na Umoja wa Mataifa dhidi ya Libya mwaka 2011 na Umoja wa Mataifa.

Katika mkutano uliofanyika katika mji mkuu wa Ujerumani, Berlin, viongozi hao kutoka nchi kumi na moja pia wamekubaliana kuachana na kuingilia kwa nchi ya kigeni katika mgogoro unaoendelea kuikumba Libya  Hata hivyo wengi wana mashaka kuhusu makubaliano hayo iwapo yatatekelezwa.