Back to top

Viongozi wa nchi zinazoendelea kukumbwa na vita washauriwa kujadiliana

08 February 2019
Share

Kamishna wa shirika la wakimbizi duniani Filippo Grand amesema ipo haja ya wakuu wa nchi ambazo zimeendelea kukumbwa na vita na kusababisha idadi ya wakimbizi kuongezeka kukaa pamoja ili kuona namna ya kutatua changamoto zinazosababisha vita.

Bw. Grandi amesema  pia wataandaa majadiliano na serikali juu ya namna bora ya kushughulikia wakimbizi hapa nchini ili kuweza kuwabaini wakimbizi wa kweli na watu wanaotumia mwanya huo ili kufanya uhalifu.