Back to top

Viongozi wawili CWT wasimamishwa kazi.

17 September 2022
Share

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CWT Mwl.Deus Gracewell Seif na aliyekuwa muweka hazina wa CWT Taifa Abubakar Salum Allaw wamesimamishwa kazi kwa kukutwa na hatia ya jinai ya matumizi mabaya ya madaraka na uchapushaji wa fedha za CWT
Kiasi cha shilingi 13,930,963.

Akizungumza Jijini Dodoma Kaimu Rais wa CWT  Dinah Mathamani amesema kupitia kikao cha dharura cha baraza la Taifa kilichofanyika septemba 15 hadi 17,2022 jijini Dodoma moja ya suala lililojadiliwa ni hukumu ya viongozi hao.


Kaimu Rais amesema viongozi hao walihukumiwa kifungo cha miezi sita na kurejesha fedha hizo za CWT  na baada ya baraza la Taifa kupokea na kujadili wajumbe waliazimia kuwasimamisha katika nafasi zao ili wawafikishe kwenye maamuzi zaidi ya mkutano Mkuu.

Kwa kipindi chote ambacho wamesimamishwa hawatahusika na shughuli zozote zinahusiana na chama cha Walimu Tanzania.