Back to top

VIPANDE 18 VYA MWILI VYAKUTWA KWENYE TANKI

06 September 2023
Share

Maafisa wa upelelezi, wanawashikilia watu wawili baada ya kugundua mwili wa mwanamke, ambaye hakufahamika jina, ukiwa umekatwa vipande 18 na kufichwa kwenye tanki la maji taka katika mtaa wa Makindye mjini Kampala nchini Uganda.

Maafisa wa polisi walibaini kiwiliwili kilichokatwa, pamoja na sehemu nyingine za mwili, na siku ya pili ya masako walikuta kichwa, huku pua wala masikio vikiwa vimewekwa kwenye chupa ya whisky iliyofukiwa mbali na eneo la tukio.

Kwa Mujibu wa Msemaji wa Polisi wa Jiji la Kampala Patrick Onyango, watu wawili wako chini ya ulinzi mama mwenye nyumba ambapo mwili wake uligunduliwa na mpangaji ambaye matone ya damu yalionekana ndani ya chumba chake.

Sehemu za siri za mwathiriwa hazikuwepo, na hivyo kusababisha uvumi kwamba wenda mauaji hayo yanahusiana na imani za kishirikisha.