Vipaumbele Bajeti Kuu 2020/2021.

Serikali imesema Bajeti Kuu ya mwaka wa fedha 2020/21 itajikita zaidi katika maeneo mbalimbali ya vipaumbele yenye kuchochea mageuzi ya uchumi na maendeleo ya watu ikiwemo kukarabati miundombinu iliyoharibiwa na Mvua Nyingi na kupambana na homa Kali ya Mapafu (COVID-19).

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Philip Mpango wakati akiwasilisha Bajeti kuu ya seriklai ya mwaka 2020/21 ikiwa ni bajeti ya tano na ya mwisho katika utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17 – 2020/21. 

Waziri Mpango amesema  serikali italazimika kuelekeza rasilimali katika kukarabati barabara, madaraja, reli na miundombinu mingine iliyoharibiwa na mafuriko  na kuendelea kupambana na athari za janga la COVID-19  kusaidia sekta zilizoathirika zaidi.