Back to top

Vishoka Songwe wahukumiwa kifungo au faini.

30 June 2020
Share

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya wilaya Ileje mkoani Songwe amewahukumu adhabu ya kifungo cha miaka 5 jela au faini ya Shilingi  laki 8  vishoka wawili waliojifanya maafisa wa TANESCO ili kuwahadaa wananchi kwa lengo la kujipatia fedha. 

Afisa Usalama wa TANESCO mkoa wa Songwe Juma Mahuba amesema vishoka hao pia walikutwa na baadhi vifaa vya umeme vya shirika hilo.