
Mwendesha mashtaka mkuu wa Ukraine amesema takriban watoto 153 wameuawa huku 245 wakijeruhiwa nchini humo tangu Urusi iivamie nchi hiyo wiki tano zilizopita ambapo amesema ofisi yake inaendelea kufuatilia ili kubaini jumla ya idadi ya watoto waliojeruhiwa huko Mariupol na pia katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Kyiv, Chernihiv na Luhansk.
