Back to top

VITI MWENDO KWENYE KITUO CHA DALADALA MUHIMBILI

18 July 2023
Share

Hospitali ya Taifa Muhimbili, imeanzisha huduma ya kubeba wagonjwa wasioweza kutembea kutoka kwenye kituo cha daladala kilichopo nje ya geti la kuingilia hospitalini hapo, hadi katika maeneo ya kutolea huduma kwa kutumia viti mwendo (Wheel chairs).
.
Akitoa taarifa hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga wa hospitali hiyo, Bi. Redempta Matindi amesema huduma hiyo inatolewa na waliokuwa waraibu wa dawa za kulevya ambao wanaendelea na tiba ya Methadone.