Back to top

Vituo bubu vinavyotoa huduma ya afya bila kuwa na sifa vyafungiwa.

14 April 2018
Share

Ofisi ya msajili wa hospitali binafsi kutoka wizara ya afya imevifungia vituo bubu viwili vya afya vikidaiwa kukosa sifa za kutoa huduma wilayani Gairo mkoani Morogoro na kuwafungulia mashitaka wamiliki wa vituo hivyo.

Msajili msaidizi wa hospitali binafsi kutoka wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia , wazee na watoto Dkt. Anthony Kyundya amesema vituo hivyo vimekuwa hatari kutokana na kushindwa kukidhi vigezo vya kiafya ambapo wengi wao wamekuwa wakifanya kazi kwenye mazingira mabovu ikiwemo kutozingatia usafi, watoa huduma kutokuwa na weledi wa kutosha na kwamba wamefungia vituo hivyo ili kulinda afya za wananchi wa Gairo na watanzania kwa ujumla.

Baadhi ya wanaodhaniwa kuwa wahusika waliokutwa katika vituo hivyo wamekana kutowafahamu wamiliki wala watoa huduma huku wananchi wakipongeza hatua hiyo ya serikali na kutaka itiliwe mkazo zaidi ili kulinda afya za watanzania na kuepusha matatizo ya kiafya yanayoweza kuzuilika.