Back to top

Vivuko na madaraja zaidi ya 15 vyasombwa na maji mkoani Ruvuma.

23 February 2021
Share

Vivuko na madaraja zaidi ya 15 katika Tarafa ya Hagati na Tarafa ya Mbuji wilayani Mbinga mkoani Ruvuma  vimesombwa na maji kutokana na mvua  zinazoendelea kunyesha na kukata mawasiliano kati ya vijiji na vijiji wilayani humo.
.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Bw. Cosmas Nshenye wakati akizungumza kwenye Baraza la Madiwani la Halmashauri ya mji wa Mbinga na kusema kuwa hali hiyo inatokana na watu kulima jirani na mito na kusababisha mito hiyo kutanuka.
.
Kwa upande wao Madiwani wa Halmashauri ya mji wa Mbinga wanasema kutokana na kusombwa na maji  kwa vivuko kunasababisha wanafunzi kushindwa kwenda shule.
.
Aidha, akizungumza kwenye kikao cha bodi ya barabara Meneja wa wakala wa  barabara za mjini na vijijini(TARURA)mkoa wa Ruvuma Mhandisi Edward Lomelo amesema vivuko na madaraja yatatengenezwa kulingana na bajeti iliyopo.