Back to top

Vivuko vinne vya watu binafsi katika kisiwa cha Ukara vyafungiwa.

10 October 2018
Share

Kufuatia sakata la abiria zaidi ya 300 katika kisiwa cha Ukara wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza kugomea usafiri wa vivuko vya Mv sabasaba na Mv ukara,serikali imeamuru abiria wote kuendelea kutumia usafiri wa vivuko hivyo, hadi hapo ujenzi wa kivuko kingine kitapojengwa huku ikivifungia vivuko vinne vya watu binafsi.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa polisi wa wilaya ya Ukerewe SP Ignatus Kapila baada ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo kufanya mkutano wa hadhara na wananchi wa kata ya Bwisya.

Vivuko vya watu binafsi vilivyofungiwa kutoa huduma ya usafiri kati ya kisiwa cha Ukara na maeneo mengine ya wilaya ya Ukerewe ni cha Katende kupitia Sizu kwenda Buguza, Bukungu kwenda Lubaga, Chifule kwenda Kakukuru na cha kutoka Kome kwenda Buguza.