Back to top

VURUGU KWA MKAPA, MMOJA ARIPOTIWA KUFARIKI

28 May 2023
Share

Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu kupitia mitandao yake ya kijamii amesema mtu mmoja, mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 40, ameripotiwa kufariki huku wengine 30 wakijeruhiwa, kufuatia vurugu zilizotokea uwanja wa mpira wa Benjamin Mkapa mkoani Dar es Salaam.
.
Mhe. Ummy amesema majeruhi wengi wana majereha madogomadogo, na wanaendelea vizuri, ambapo amesema timu ya wataalam wa huduma za dharura ya Hospitali ya Taifa Muhimbili imeshawasiliana na Hospitali ya Rufaa Ya Mkoa wa Temeke na wapo standby kupokea na Kuwahudumia majeruhi wanaohitaji matibabu zaidi.