Back to top

Vuta nikuvute ujenzi kituo cha polisi Kisaki, Morogoro.

22 August 2019
Share

Mvutano umeibuka miongoni mwa wananchi wa kata ya Kisaki wilaya ya Morogoro juu ya kujengwa kwa kituo cha polisi na kituo cha afya katika eneo la kijiji cha Kisaki stesheni baada ya baadhi ya wakazi wa vijiji vingine vya kata hiyo kutaka vituo hivyo vijengwe katika eneo lenye idadi kubwa ya wananchi kuliko mahala vinakojengwa kwa sasa huku wengine wakieleza eneo hilo ni sahihi. 

Wananchi wa Kisaki wameyasema hayo katika eneo kinapotarajiwa kujengwa kituo cha afya wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa wa Morogoro Dakta Kebwe Stephen Kebwe ya kukagua miradi ya maendeleo ambapo wameshukuru serikali kwa kutatua kero ya ukosefu wa huduma za afya na usalama wa raia na mali zao ambayo kwa muda mrefu kulikuwa hakuna huduma hizo.

Mkuu wa wilaya ya Morogoro bi, Regina Chonjo aliyeambatana na dakta kebwe katika ziara hiyo amebainisha hatu zilizofikiwa mpaka sasa ikiwa ni pamoja na kupatiwa kiasi cha fedha shilingi milioni 400 ikiwa ni ahadi ya Rais Dakta John Pombe Magufuli kwa ajili ya ujenzi huo.

Kufuatia sintofahamu iliyopo miongoni mwa wananchi wa vijiji vya kata ya Kisaki mkuu wa mkoa wa Morogoro Dakta Kebwe Stephen Kebwe anatoa ufafanuzi juu ya agizo la ujenzi wa vituo hivyo katika eneo la kijiji cha Kisaki Stesheni ambapo ameeleza maagizo ya rais hayatapuuzwa kilichopo ni utekelezaji na wala hakuna atakaye pingana na agizo hilo.