
Vyama saba vya kisiasa nchini Afrika Kusini, vimetia saini mkataba wa kufanya kazi pamoja ili kukiondoa madarakani chama tawala cha African National Congress (ANC), kinachoongozwa na Rais wa nchi hiyo, Cyril Ramaphosa, katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka 2024, ambapo kulingana na mkataba huo vyama hivyo vitafanya kazi pamoja, ikiwemo kugawana nyadhifa za uongozi katika nafasi mbalimbali zikiwemo za Mawaziri.
.
Pia vyama hivyo vimelenga kukizuia chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) cha Julius Malema, ambacho ni cha tatu kwa ukubwa nchini humo, kupigiwa kura ili kuingia madarakani, huku wachambuzi wa kisiasa wakidai kuwa Chama cha ANC kiko hatarini kupoteza wabunge wake wengi kwa mara ya kwanza tangu Afrika Kusini irejee kwenye demokrasia mwaka 1994.
.
Makubaliano hayo yanakuja wakati nchi hiyo ikikabiliana na hali mbaya ya uchumi, ufisadi, ukosefu wa ajira na mzozo wa nishati.
