
Msajili wa Vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, amevitaka vyama vipya 18 vya siasa vilivyotuma maombi ya usajili kwenye ofisi yake kuwa na subira, kwani mchakato wa kuvisajili hauwezi kuendelea, mpaka pale uhakiki wa vyama vilivyopo utakapokamilika.
.
Jaji Mutungi ameyasema hayo kwenye mkutano wa kikao kazi na viongozi wa vyama vya Siasa nchini ikiwa ni maandalizi ya kuelekea kwenye uhakiki wa vyama hivyo.
