Back to top

Vyama Vya Upinzani Uganda vyaapa kuzuia wizi wa kura.

12 January 2021
Share

Wagombea wakuu wa upinzani katika uchaguzi wa Alhamisi nchini Uganda wameazimia kushirikiana katika kulinda kura zao kwa pamoja. Aidha wamefafanua kuhusu mkakati wao wa kumuunga mkono mwenzao atakayepata kura nyingi ikiwa uchaguzi huo utaingia katika duru ya pili.
.
Mgombea wa chama cha NUP, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, mgombea wa FDC Patrick Oboi Amuriat na jenerali Mugisha Muntu wa ANT wamesisitiza kwamba uchaguzi huu ni muhimu sana kwa Uganda na watafanya kila juhudi kulinda kura zao kwa pamoja.
.
Hii ni kwa sababu wana imani kwamba rais Museveni mara hii hawezi kupata asli mia 50 na kura moja ili kutangazwa mshindi wa duru ya kwanza.

DW