Back to top

Vyama vya ushirika wilaya ya Tunduru vyanunua magari

14 July 2020
Share

Vyama vitatu vya vya msingivya ushirika( AMCOS) vya Mtiti,Mruji na Sama vimenunua magari  kila chama gari moja  ili kutatua changamoto ya kusafirisha mazao iliyokuwa ikivikabili vyama hivyo.

Mwandishi wa Mruji (AMCOS) Bw. Zuberi Chiwale amesema kuwa magari hayo yaliyotumika yote matatu yamenunuliwa  kwa shilingi milioni 135 za mapato ya ndani ya vyama hivyo.

Kwa upande wake mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika wa mkoa wa Ruvuma Bi.Bumi Masuba amesema ununuzi wa magari hayo ni mwelekeo mzuri wa kukuza uchumi wa vyama  hivyo.

Akizindua magari hayo mkuu wa wilaya ya Tunduru Bw.Julius Mtatiro amepongeza hatua hiyo kubwa ya maendeleo na kusema unaviweka vyama  vya ushirika kwenye mwelekeo mzuri.