Back to top

Waandishi waandamana kuataka kuachiwa kwa mwandishi mwenzao Arusha.

14 March 2019
Share

Waandishi wa habari jijini Arusha wamekusanyika kituo cha polisi kushinikiza kuachiwa kwa mwandishi mwenzao Basil Elias ambaye anashikiliwa na polisi baada ya kufuatilia tukio la wananchi kuugua magonjwa ya matumbo kwa kile kinachodaiwa kusababishwa na maji.

Akizungumza na ITV mwandishi wetu aliyepo jijini Arusha Asraji Mvungi, ametueleza kuwa kwa takribani wiki moja sasa kunatatizo la mlipuko wa watu kuugua magonjwa ya matumbo ambao unahusishwa na maji jijini humo, licha ya mamlaka zinazohusika na maji kuonekana zikitoa maelezo ambayo yanapingana na hali halisi.

Hata hivyo maelezo ya mamlaka ya maji na mamlaka ya mkoa yameeleza kwamba zimekiri kwamba kuna tatizo hilo la maji la watu kulalamikia kwamba maji yana matatizo na watu wanaugua matumbo, lakini wamesema wanaendelea na uchunguzi licha ya kupata taarifa hizo.
Kufahamu zaidi Bonyeza Video hapo chini->