
Wabunge wa Bunge la Muungano wameitaka serikali iweke mikakati na bajeti maalum itakayo wezesha kudhibiti mlipuko wa wadudu waharibifu wa mimea aina ya viwavi jeshi vamivi ambao wanaenea kwa kasi kubwa nchini na kufifisha ndoto za wakulima kupata mazao ya kutosha.
Wabunge wametoa kauli hiyo wakati wakizungumza na watalaam wa viuatilifu kutoka TPRI na Mamlaka ya kudhibiti ubora wa mbolea nchini TFRA waliyokuwa wanatoa elimu kwa wabunge juu ya madhara ya viwavi jeshi matumizi sahii ya viatilifu na mbolea kwa wakukima.