Back to top

Wachangiaji wa Damu kuzawadiwa jezi mpya za Simba na Yanga.

11 July 2020
Share

Kuelekea mechi ya watani wa jadi kati ya Simba na yanga siku ya Jumapili, Taasisi ya tiba ya Mifupa(MOI) kwa kushirikiana na Azim Dewj pamoja na GSM imezindua kampeni ya kuchangia damu ambapo mchangiaji atapatiwa jezi mpya ya Timu anayoishabakia.

Kampeni hiyo inayokwenda kwa jina la "Changia Damu Okoa Maisha Upate Jezi" inalenga kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa damu salama kwa majeruhi wa ajali, watoto wenye vichwa vikubwa, wagonjwa wasiofahamika na wasio na ndugu pamoja na wagonjwa wengine wasio na ndugu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tiba MOI Dkt.Samwel Swai amesema mahitaji ya damu MOI ni chupa 30 kwa siku ambapo kumekuwa na changamto ya upatikanaji wa damu kutokana na kupungua kwa wachangiaji wa hiari.

Dkt.Swai amesema zoezi la uchangiaji damu litakuwa siku ya Jumamosi tarehe 11/07/2020 katika eneo la kuegesha magari kitengo cha dharura cha zamani ambapo zoezi litaanza saa tatu asubuhi mpaka saa kumi jioni.