
Meneja wa Idara ya Habari Simba SC Ahmed Ally amesema katika mchezo wao wa Jumapili dhidi ya Power Dynamos, utakao chezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, wachezaji wake watatu watakosekana kwenye mchezo huo, ambao ni Aishi Manula, Henock Inonga na Aubin Kramo.
Ahmed Ally amesema kikosi kimefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Azam Complex pale Chamazi kwa ajili ya kuzoea uwanja, kwani tangu wameanza msimu huu hawajawahi kutumia uwanja huo, licha kwamba Wapo wachezaji wa timu hiyo wanaujua uwanja na wengine hawaujui.
Mchezo wa Simba SC dhidi ya Power Dynamos utachezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex Jumapili Oktoba mosi saa 10:00 jioni.
