
Wachezaji wa timu ya Taifa ya Gambia wamenusurika kifo baada ya ndege waliyokuwa wakiitumia, kuelekea Ivory Coast, kushiriki fainali za AFCON, kupata hitilafu kwenye mfumo wa usambazaji hewa ya Oksijeni, dakika 10 tu baada ya kuruka.
.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Kampuni inayomiliki ndege hiyo ya Air Cote d'Ivoire imesema kuwa inafanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha hitilafu hiyo.
.
Hata hivyo Kocha wa timu hiyo Tom Saintfiet amempongeza Rubani wa ndege hiyo kwa kuchukua hatua ya haraka ya kusitisha safari, ambayo imeokoa maisha yao.
