Wachimbaji wa dhahabu walalamikia tozo mgodini.

Wachimbaji wadogo wa dhahabu waliopo kwenye mgodi wa Lundamilo uliopo tarafa ya Kwekivu wilayani Kilindi mkoani Tanga wamelalamikia tozo na michango wanayotozwa kwenye mgodi huo bila kupewa risiti na hivyo kuiomba serikali kuingilia kati suala hilo.
.
Wachimbaji hao wa mgodi wa Lundamilo wameyasema hayo baada ya kamati ya ulinzi na usalama ikiongozwa na mkuu wa wilaya ya Kilindi kufika kwenye mgodi huu ili kusikiliza kero za wachimbaji hawa wakiwemo wakina mama.
.
Kwa upande wa wachimbaji wakina nao wamedai kuwa vifaa wanavyo tumia ni duni hivyo wameiomba serikali kuwafikiria wakina mama hao ili waweze kutumia vifaa vya kisasa ambavyo vitasaidia kuondokana na uchimbaji wa kizamani wa kutumia dhana duni.
.
Baada ya kusikiliza kero hizo za wachimbaji wapatao elfu mbili waliopo kwenye mgodi huu mkuu wa wilaya ameahidi kuunda tume itakayo chunguza changamoto hizi zilizopo kwenye mgodi huu.