Back to top

Wachimbaji wa madini waliovamia mgodi wapewa siku mbili kuondoka.

21 January 2021
Share

Naibu Waziri wa Madini Mhe Prof Shukrani Manya ametoa siku mbili kwa wachimbaji wadogo madini wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 300 waliovamia eneo lenye leseni ya mgodi wa madini ya Alimasi wa El-Hilal wilayani Kishapu mkoani Shinyanga kuondoka katika eneo hilo.

Pia amemuagiza Afisa madini mkazi wa mkoa wa Shinyanga Mhandisi Joseph Kumburu kuandaa utaratibu wa kuwasajili wachimbaji hao katika vikundi na kuwapa maeneo mengine ya uchimbaji.