Back to top

WACHIMBAJI WADOGO WAFAIDIKE FURSA ZA UCHIMBAJI MADINI.

20 April 2022
Share

Serikali imetoa wito kwa Halmashauri za Mikoa katika maeneo ambayo tafiti za uchimbaji Madini zinapokamilika kuhakikisha wanatenga maeneo na kuboresha miundombinu rafiki kwa wachimbaji wadogo kupata nafasi ya kuchimba Madini.

Naibu Waziri wa Madini Dkt.Steven Kiruswa amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Urambo, Margaret Sitta aliyeuliza juu ya Mkakati wa serikali katika kusaidia wachimbaji wadogo wa madini kufaidika na shughuli za kiuchumi katika maeneo yanayowazunguka