Back to top

Wachimbaji wadogo waiomba serikali kuwatatulia mgogoro mkoani Iringa

15 January 2019
Share

Wachimbaji wadogo wa dhahabu katika mgodi wa Ulata  wameiomba serikali kuingilia na kumaliza mgogoro uliopo katika mgodi huo ili kuwezesha mmiliki halali wa mgodi huo kuingia na kufanya kazi hivyo kunusuru ajira za wachimbaji wadogo.

Wakizungumza kwenye mkutano na naibu waziri wa madini Stanslaus Nyongo aliyetembelea mgodi huo wachimbaji hao wamesema wanashindwa kufanya kazi na kufikia malengo kutokana na mgodi huo kuwa katika mgogoro kwa muda mrefu licha ya mmiliki mwenye leseni ya mgodi huo kushinda kesi mahakamani na kukabidhiwa mgodi rasmi.

Kwa upande wake mmiliki wa mgodi huo bwana Ibrahimu Msigwa amesema ameshindwa kufanya uwekezaji ili kuufanya mgodi kuanza kuzalisha kutokana na mgogoro uliopo kwenye mgodi huo hivyo kumfanya kushindwa kuendeleza.