Back to top

Wachukua taarifa za kijiografia wakemewa

19 May 2022
Share

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bw.Kaspar Mmuya amekemea tabia ya wachukua taarifa wasio waadilifu wanaochukua taarifa za kijiografia (GPS) za sehemu moja na kuzitolea taarifa kwenye eneo jingine, Jambo ambalo linaharibu kazi data na linaweza kupelekea mfumo kutoa taarifa zisizosahihi ambapo amewasisitiza watendaji kukagua na kujiridhisha hasa pale inapotokea taarifa hizo kufanana eneo moja na jingine.
.
Bw.Mmuya amesema hayo ziara yake ya kukagua utekelezaji wa operesheni ya anwani za makazi katika wilaya ya Kilwa na Rufiji.