Back to top

WAENDESHA BODABODA 4 WAUAWA MKOANI MARA

28 May 2023
Share

Watu wanne, wanaume ambao ni waendesha bodaboda, wanaokadiliwa kuwa na umri wa miaka 26 nadi 30, wameuawa kwa kushambuliwa na vitu vyenye ncha kali usiku wa kuamkia leo katika Kijiji cha Nyakiswa kilichopo Kata ya Kyanyari, wilayani Butiama, mkoani Mara.
.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi (CP) Awadhi Juma amethibitisha kutokea kwa tukio ambapo amesema wanaendelea na uchunguzi ili kuwabaini wahalifu waliohusika na tukio hilo.