Back to top

WAFANYA VURUGU, WAKIDAI WENZAO WAMEZAMISHWA MAJINI

23 May 2023
Share

Watu 12 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Arusha, kufuatia umati wa wavuvi katika Kitongoji cha Jangwani, kilichopo eneo la Mto wa Mbu, wilayani Monduli kuzusha vurugu na kufanya uharibifu wa ofisi ya Kijiji, ikiwemo kuvunja madirisha na kuchana bendera ya Taifa, wakidai kuwa wavuvi wenzao wamezamishwa kwenye maji wakati wanakamatwa na Askari wa Uhifadhi.
.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Justine Masejo ambapo amebainisha kuwa vurugu hizo zilianza baada ya Askari wa Uhifadhi waliokuwa doria, kuwakamata wavuvi watatu waliokuwa wakivua samaki kwenye maeneo yaliyozuliwa.