Back to top

Wafanyabiashara 10 Mbaroni utoroshaji madini bila kibali.

09 September 2019
Share

Watu 10 wanaodaiwa kuwa ni wafanyabiashara wa Madini wamefikishwa Mahakani kwa kosa la kutorosha madini ya Dhahabu.

Watano kati yao wamesomewa mashtaka ya kujipatia fedha kwa udanganyifu, utakatishaji fedha na kukutwa na dhahabu bila kuwa na Kibali, huku wengine watano wakiwekwa chini ya uangalizi wa Mahakama kwa kipindi cha miezi 12 na kutakiwa wawe na tabia njema. 

Miongoni mwa wafanyabishara hao yumo mmiliki wa mabasi ya Sauli, yanayofanya safari zake kati ya Mbeya na Dar es Salaam, Sauli Solomoni.