Baadhi ya wafanyabiashara wa maembe kutoka Jijini Dar es Salaam wamegoma kununua maembe ya wakulima wa Kwediboma wilayani Kilindi mkoani Tanga wakidai kuwa ushuru shilingi 300,000/= wanaotozwa na Halmashauri ya Wilaya hiyo kwa gari moja aina ya Fuso ni mkubwa kwao hali iliyopelekea maembe kuozea shambani na kuwaathiri zaidi wakulima.