Back to top

Wafanyabiashara watatu Ruvuma mbaroni kwa kuficha mafuta ya kula.

14 May 2018
Share

Wafanyabiashara watatu wilayani Songea mkoani Ruvuma wanashikiliwa na polisi kwa kuficha mafuta ya kula na kufanya bidhaa hiyo iadimike huku kati yao akificha zaidi ya ndoo 700 za lita 20 za mafuta ya kula katika ghala bubu na bidhaa nyingine zikihifadhiwa chooni.

Baada ya kufanya ukaguzi katika maghala ya kuhifadhi bidhaa za vyakula Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bi.Christine Mndeme amebaini wafanyabiashara kuhifadhi bidhaa za vyakula katika maghala yasiyosajiriwa na pia kuficha mafuta ya ndoo za lita 20 ndoo 959 na ndoo za lita kumi ndoo 3200 na kuagiza Jeshi la Polisi kuwashikilia wafanyabiashara walioficha mafuta ya kula.

Wafanyabiashara wanaoshikiliwa na polisi kwa kuficha mafuta ya kula na kuhifadhi bidhaa kwenye maghala yasiyosajiliwa ni Oscar Ngao anayedaiwa kuficha mafuta ya kula ndoo 759 na bidhaa nyingine kuhifadhi chooni,Mfanyabiashara Narendre Red anashikiliwa kwa kuficha  mafuta ya ndoo 10 lita 3200 na Sokor Maria anashikiliwa kwa kuficha mafuta ndoo za lita 1o 400 na za lita 20 200.

Hivi karibuni Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa akizungumza Bungeni jijini Dodoma aliwaonya wafanyabiashara kuacha kuficha mafuta ya kula na kusababisha yapande bei na kuadimika mitaani kwamba watachukuliwa hatua.