Back to top

Wafanyabiashara wawili matatani kwa wizi wa maji Mwanza.

16 May 2020
Share

Mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira jijini Mwanza “MWAUWASA” imeendesha operesheni maalumu usiku wa manane iliyolenga kuwabaini watumiaji wa  maji ya mamlaka hiyo kinyemela na kufanikiwa kuwakamata watu wawili wanaoendesha biashara ya kuuza maji na kuosha magari  kwa kutumia maji ya mamlaka hiyo kinyume na utaratibu.

Watuhumiwa hao wa wizi wa maji wamekamatwa katika eneo la Mkolani na Buhongwa jijini humo baada ya kikosi kazi cha watendaji wa mamlaka hiyo kilichoongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa mamlaka hiyo jijini Mwanza Mhandisi Leonard Msenyele kuamua kufuatilia na kudhibiti upotevu wa maji.