Back to top

Wafanyakazi ofisi za serikali wapunguzwa Zimbabwe.

26 January 2021
Share

Huduma za serikali nchini Zimbabwe zimeathiriwa pakubwa baada ya amri ya kufunga baadhi ya shuguli za kawaida ili kupunguza mambukizi ya virusi vya corona wakati idadi ya vifo iliongezeka nchini humo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, taifa hilo la kusini mwa Afrika limefungiwa shuguli za kawaida tangu Januari, wakati wiki iliopita serikali ikitoa amri kwamba asilimia 10 pekee ya wafanyakazi wa serikali wawe ofisini ili kuzuia maambukizi.

Janga hilo limeathiri maafisa wa ngazi za juu serikalini ambapo tayari mawaziri wanne wamefariki, watatu miongoni mwao wakifa katika kipindi cha wiki mbili zilizopita. Ofisi nyingi za serikali zilionekana tupu kuanzia Jumatatu, wakati maafisa wa dharura pekee wakibaki.

#VOA