
Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amewataka wafugaji na wakulima kufuata taratibu ili kuepusha migogoro, huku akisema wakulima ni Watanzania na Wafugaji ni Watanzania hivyo Kitu muhimu na cha msingi ni kufuata taratibu.
Waziri Mkuu amebainisha haya Mkoani Tanga katika wilaya ya Handeni, ambapo alipata fursa ya kuongelea suala la mgogoro wa wakulima na wafugaji na kupata wasaa wa kusikiliza migogoro ya wakulima na wafugaji ambapo mkulima Bw. Omari Athumani, mkazi wa Jimbo la Mkata Mashariki alieleza kero za wafugaji kulisha mifugo kwenye mashamba ya wakulima.
Akizungumzia Sekta ya Kilimo kuhusu hoja iliyotolewa na mkulima huyo, Waziri wa Kilimo Mhe. Daniel Chongolo, amesema "mifugo ni sehemu ya wakulima katika mazingira ya kazi na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, imeongea na Waziri Mwenzangu Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Kakurwa ili kwa kushirikiana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupima na kutenga maeneo rasmi kwa ajili ya wakulima na wafugaji katika kuondokana na kero zao" Amesema Waziri Chongolo.
Kadhalika Waziri Mkuu Nchemba ameelekeza anayefanya kosa kama mfugaji hatua za kisheria zichukuliwe kwa aliyehusika na sikuhukumu jamii yote ya wafugaji, "Ukitokea umeteleza usifanye kiburi, hakuna ubabe na jeuri katika kuvunja sheria, kila mmoja afanye shughuli ya maendeleo kwa kuzingatia sheria, katiba na undugu"

