Back to top

Wafugaji walalamikia ukosefu wa soko la Ngozi wilayani Shinyanga.

12 November 2018
Share

Wafugaji wa Ng’ombe,Mbuzi na Kondoo wilayani Shinyanga wamelalamikia ukosefu wa soko la ngozi na kuiomba serikali iwasaidie kupata soko la uhakika la mazao yanayotokana na mifugo.

Wananchi hao wamesema wamekuwa wakikatishwa tamaa na baadhi ya maofisa wa serikali kuwapuuzia pale wanapowasilisha kero kwao hali ambayo imekuwa ikisababisha baadhi ya watu wasio waaminifu kutumia mwanya huo kutorosha ngozi nje ya nchi na serikali kukosa mapato.

Wakizungumzia hali hiyo baadhi ya wafugaji wa ng’ombe,mbuzi na kondoo wilayani Shinyanga wamesema serikali imekuwa ikikosa mapato kufuatia ngozi inayozalishwa baada ya mifugo kuchinjwa kukosa soko.

Kwa upamde wake afisa biashara wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Bw.Petro Matulanya amesema soko la ngozi lipo ambapo amewaelekeza wafugaji soko lilipo na kumuagiza afisa mifugo wa halmashauri hiyo kushirikiana na wafugaji kuhakikisha ngozi zote zinazozalishwa zinafika sokoni.