Back to top

Wafungwa 11 wapoteza maisha kwa kukosa chakula na dawa DRC.

08 January 2020
Share

Wafungwa 11 wamepoteza maisha katika gereza kubwa la Makala jijini Kinshasa nchini DRC tangu kuanza kwa mwaka 2020,ripoti zinaonyesha vifo hivyo vimesababishwa na uhaba wa chakula na dawa katika gereza hilo.

Wafungwa watatu walipoteza maisha siku ya Jumatatu, baada ya kukosekana kwa dawa za kuwatibu na familia zao zilishindwa kuwasaidia.

Afisa wa juu katika gereza hilo ambaye hakutaka jina lake kutajwa amesema kuwa, hali imekuwa mbaya kwa sababu tangu mwezi Oktoba mwaka uliopita, serikali haijatoa fedha za kulisaidia gereza hilo kununua dawa na chakula.