Back to top

Wafungwa 130 waachiwa katika gereza Kuu la Ukonga Dar es Salaam.

10 December 2019
Share

Siku moja baada ya Rais Dkt.John Pombe Magufuri kuwasamehe wafungwa 5533 katika maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru, wafungwa 130 miongoni mwao waliokuwa wafungwa katika gereza kuu la Ukonga Dar es Salaam wameachiwa leo.

Akizungumza wakati wa kuwaruhusu wafungwa hao Mkuu wa Magereza ya Dar Es Salaam, Kamishna wa Magereza Julius Ntambala amewataka kuhakikisha wanabadilika na kuishi kwa kufata sheria na taratibu za nchi.

Kati ya wafungwa wote 5533 walioachiwa kwa msamaha wa Rais Jumla ya wafungwa 293 wanatoka katika magereza ya jiji la Dar Es Salaam.