
Waganga wafawidhi wa Hospitali zote nchini, wametakiwa kuwajibika na kuacha kufanya kazi kwa mazoea, ili kuleta tija ya uwekezaji uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, katika sekta ya afya.
.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, alipofanya ziara katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, kuangalia hali ya utoaji huduma za afya na kufanya mazungumzo na Wakuu wa Taasisi za Afya, ikiwemo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Taasisi ya Mifupa (MOI), Bohari ya Dawa (MSD), Shirika la Bima la Taifa (NHIF), Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA), Mganga Mkuu wa Mkoa na Waganga Wafawidhi wa Hospitali za Rufaa za Mkoa wa Dar es saalam.
.
Dkt. Mollel amesisitiza kuwa, Serikali haitamvumilia Kiongozi yoyote anayekwamisha juhudi za uboreshaji wa huduma katika sekta ya afya nchini kwani Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mapinduzi makubwa katika sekta ya afya hivyo ni jukumu la usimamizi imara, ili kuleta ubora wa Huduma kwa wananchi.