
Waganga wakuu wa Mikoa, Waganga Wakuu wa Wilaya pamoja na waganga wafawidhi wa Hospitali kwa ngazi zote nchini, wametakiwa kuzingatia maelekezo ya Mwongozo wa kutozuia maiti na kuhakikisha wananchi hawapati vikwazo vinavyoweza kuchelewesha marehemu kuzikwa.
.
Maagizo hayo yametolewa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Mhe. Muharami Shabani Mkenge, aliyetaka kujua kuhusu mpango wa Serikali wa kusamehe gharama za matibabu kwa marehemu ili kupunguza maumivu kwa wafiwa.
.
Mhe.Mollel ameendela kusisitiza kuwa Serikali ilishatoa maelekezo kwa vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini kupitia waraka namba moja wa mwaka 2021 wa kutozuia maiti na kuweka utaratibu wa kulipia gharama za matibabu na madeni ya miili.
