Back to top

Wagonjwa 45 wamelazwa kwa kusadikika kula chakula chenye sumu Dodoma.

16 December 2019
Share

Akizungumza hospitalini hapo mganga mkuu mkoa wa Dodoma Best Magoma amethibitisha kupokelewa wagonjwa hao wakiwemo watoto,wanawake na wanaume saba ambao wanaharisha na kutapika.

Mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Bw.Patrobasi Katambi akizungumza mara baada ya kutembelea majeruhi amesema kuwa tayari wameunda timu ambayo imeenda kuchukua mabaki ya vyakula kwa ajili ya kupima ili kubaini kama ni sumu kuvu au ni ile ya kuwekwa na mtu.

kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amebainisha idadi ya wagonjwa waliofikishwa katika hospitali hiyo ni 45 na kuongeza kuwa idadi hiyo inaweza kuongezeka.