Back to top

Wahalifu wa tukio la Chanika wakamatwa.

27 April 2022
Share

Kufuatia kuibuka kwa kikundi cha vijana wenye umri kati ya miaka 14 hadi 21 kufanya vitendo vya kihalifu ikiwemo kujeruhi na kuvunja nyumba mitaa ya Chanika Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Jumanne Muliro amesema tayari baadhi ya wahalifu wamekamatwa na kuahidi kuwa kila aliyeshiriki katika tukio hilo atashughulikiwa kisheria.

Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam, ACP Muliro J. Muliro ameyasema hayo alipofanya kikao Maalum na Wananchi wa Kata ya Chanika na Zingiziwa kwa lengo la kujadili masuala ya kiusalama ya maeneo hayo.

Watu 23 walikumbwa na kadhia hiyo na walipatiwa matibabu katika Kituo cha afya cha Chanika na hospitali ya Amana na baadae kuruhusiwa.

Wakazi hao walimweleza Kamanda kuwa kundi hilo la vibaka ni vijana wanaishi miongoni mwao na wengine walikwishakamatwa siku za nyuma na wamemaliza vifungo vyao na wengine wameachiwa huru kwa mujibu wa sheria.