Back to top

Wahamiaji haramu 19 raia wa Tanzania watupwa jela miezi miwili.

11 December 2019
Share

Wahamiaji haramu 19 raia wa Tanzania wamehukumiwa miezi miwili Gerezani na kulipa faini ya Shilingi Elfu Hamsini waliokuwa wamezamia kwenda nchini Afrika Kusini kinyume na sheria.

Hukumu hiyo, imesomwa na Hakimu Mkazi, Victoria Mwaikambo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya washitakiwa hao kusomewa mashitaka yao na Mawakili wa Idara ya Uhamiaji Tanzania, Shija Sitta na Godfrey Ngwijo.

Washitakiwa hao walisomewa maelezo ya makosa yao kisha wakakiri mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mwaikambo.